Vyeti vya Abdulswamad vyazua utata katika kinyang'anyiro cha ugavana kaunti ya Mombasa.

 





Mpiga kura wa Mombasa Wycliffe Ouma Ayecho ameiandikia Halmashauri ya Kitaifa inayohusiana na ukaguzi wa vyeti nchini "Kenya National Qualifications Authority" akihoji uhalali wa vyeti vya kitaaluma vya wanaowania ugavana katika kaunti hiyo.

Katika siku za hivi majuzi, imedaiwa kwenye mitandao ya kijamii, magazeti na mitandao mingine ya kielektroniki kwamba baadhi ya wagombeaji wa ugavana Kaunti ya Mombasa hawana shahada na wanapanga kutumia stakabadhi ghushi ili kupata uteuzi wao ili kujiunga na wagombea wengine katika uchaguzi ujao.


Kuruhusu wanasiasa wa aina hii wafanye mambo yao ni kinyume cha sheria na pia ni matumizi mabaya ya mfumo wetu wa uchaguzi.

Swala hili pia huwapotosha wapiga kura na kuwafanya wawachague viongozi walaghai katika afisi ya heshima ya gavana." Ilisoma sehemu ya barua yake iliyoonekana na CoastPlus.

Kwa mujibu wa kifungu cha 22 cha sheria ya uchaguzi, 2011 kanuni ya 47 ya kanuni za uchaguzi (Mkuu) wa 2012, mtu anaweza kuteuliwa kuwa mgombeaji wa uchaguzi kama gavana wa Kaunti ikiwa ana shahada kutoka chuo kikuu kinachotambulika nchini Kenya.

Katika ombi lake, Ayechoanaitaka taasisi husika kuchunguza kartasi za Abdulswamad Sharif Nassir.

Nassir ni mmoja kati ya wanaoongoza katika kinyang'anyiro cha ugavana Kaunti ya Mombasa.

Ayecho anatilia shaka shahada ya biashara ya Abdulswamad kutoka chuo kikuu cha Inoorero ambayo aliipata 2014, kulingana na bwana Ayecho, chuo hicho kilifungwa kwa madai ya kutoa vyeti ghushi.

Aidha anasema kuwa, chuo cha Inoorero kilikuwa kikitoa vyeti kwa ushirikiano na JKUAT na anadai kuwa Abdulswamad hakuwa kwenye orodha ya wahitimu wa JKUAT mwaka wa 2014.


 

Comments

Post a Comment