Polisi Mjini Mombasa wanasa gari lenye silaha hatari linalohusishwa na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir.


Polisi mjini Mombasa wamenasa gari lililokuwa na silaha hatari ambalo linamilikiwa na mshirika mkuu wa mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir.

Gari hilo ambalo nambari yake ya usajili ni KCZ 134H linamilikiwa na mgombea MCA wa wadi ya majengo Shufat Mohamed.


Kulingana na maafisa wa usalama, polisi walibaini kuwa timu ya viongozi hao ilikuwa imepanga kusababisha fujo wakati wa uteuzi wakati wa kura ya mchujo ya ODM itakayofanyika Aprili 6.

Gari hilo aina ya Toyota Probox ambalo lina chapa ya picha zote mbili za Nassir na Shufat limezuiliwa katika kituo cha polisi cha Makupa.





Mgombea huyo ameitwa na polisi ili kurekodi taarifa kuhusu tukio hilo.

Polisi wanahitaji kujua kwa nini amebeba silaha ghafi kwenye gari lake ambalo limeonekana likizurura ndani ya mji.

Hata hivyo, Nassir amepiga simu mara kadhaa kuwarai maafisa wa polisi waachilie gari hilo na kuruhusu majadiliano.

 


Comments

Post a Comment