ODM yarejesha ada ya uteuzi kwa Suleiman Shabhal



Chama cha ODM kimemrudishia mfanyabiashara Suleiman Shabhal Ksh 500,000, CoastPlus imebaini. Pesa hizo zilikuwa ada za uteuzi wa wadhifa wa ugavana, ambazo umemwendea mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir.

Chama hicho kilimpa Shahbal chaguo la kugombea Ubunge au useneta lakini mfanyabiashara huyo anaripotiwa kukataa.

Kwa mujibu wa mdokezi wetu aliye karibu na chama hicho na ambaye jina lake litaendelea kusalia sirini kwa sababu za kiusalama, kura tatu za maoni zilionyesha kuwa, Abdulswamad Shariff Nassir ndiye mgombea anayependelewa zaidi na wakaazi wa Kaunti ya Mombasa.


Bodi ya kitaifa ya uchaguzi ya chama cha ODM katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alasiri ya leo, ilithibitisha kwamba chama hicho kitatoa tikiti za moja kwa moja kwa wagombeaji maarufu kote nchini.

Chama hicho kimeamua kutumia matokeo ya kura za ndani kwa ndani ili kupima umaarufu wa baadhi ya wagombea wakuu.

Wakati huo huo, huko Siaya, James Orengo sasa atapata tikiti ya chama baada ya mpinzani wake Nicholus Gumbo kujiondoa na kujiunga na UDM, chama kinachohusishwa na Gavana wa Mandera Ali Roba.

UDM ni miongoni mwa vyama tanzu vya Azimio.


 

Comments

Post a Comment